1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Mwito kumaliza mgomo nchini Ufaransa

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImX

Serikali nchini Ufaransa imetoa mwito kwa vyama vya wafanya kazi kumaliza mgomo wa treni.Waziri wa Ajira wa Ufaransa,Xavier Bertrand amesema, majadiliano ya pande tatu,yaani kati ya serikali, vyama vya wafanyakazi na shirika la reli yataweza kufanywa ikiwa mgomo huo utamalizwa.

Wafanyakazi wa reli wanapinga hatua inayotazamia kuondosha sheria maalum inayohusika na malipo ya uzeeni kwa wafanyakazi wa serikalini wapatao milioni 1,6.Wakati huo huo wanafunzi pia wanaandamana kupinga mpango wa kujilipia masomo yao na unaotaka kuijumuisha zaidi sekta binafsi ya biashara kugharimia shule za mafunzo ya kazi.