1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Orodha ya wagombea yatajwa.

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHN

Baraza la katiba la Ufaransa limetoa orodha rasmi ya wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa rais mwezi ujao. Watu hao 12 ni pamoja na Nicolas Sarkozy wa chama cha kihafidhina cha mrengo wa kulia, msoshalist Segolene Royal na Francois Bayrou wa mrengo wa kati.

Kiongozi mwenye msimamo mkali wa kulia Jean- Marie Le Pen pia amepitishwa katika orodha hiyo, baada ya kukusanya maidhinisho 500 yanayohitajika.

Majina ya wagombea hao 12 yatachapishwa katika gazeti rasmi la serikali leo, ambapo televisheni na radio zitatakiwa kutoa nafasi sawa za matangazo kwa kila mgombea kabla ya kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Aprili 22.