1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Royal aonya kutokea ghasia nchini Ufaransa.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4j

Mgombea wa kiti cha urais nchini Ufaransa kutoka chama cha Kisoshalist Segolene Royal , ameonya kuwa Ufaransa inaweza kukabiliwa na wimbi la ghasia katika maeneo ya vitongoji vyake iwapo Nicolas Sarkozy wa chama cha kihafidhina cha UMP anashinda uchaguzi wa kesho Jumapili wa duru ya pili.

Royal ameiambia radio RTL kuwa Sarkozy ataipeleka Ufaransa katika mfumo wa ukatili.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani alikosolowa kwa kuwaeleza vijana waliokuwa wakiandamana kuwa ni takataka kabla ya machafuko ya mwaka 2005 ambayo yaliyakumba maeneo kadha ya vitongoji katika miji ya Ufaransa. Kura ya maoni inampa Sarkozy ushindi wa kiasi cha asilimia 8 ya kura dhidi ya Royal.