1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy ameshinda uchaguzi wa rais nchini Ufaransa

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4A

Mgombea uchaguzi wa kihafidhina,Nicolas Sarkozy ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya Jumapili nchini Ufaransa. Sarkozy aliekuwa waziri wa ndani amemshinda mpinzani wake wa chama cha kisoshalisti Segolene Royal kwa kujinyakulia asilimia 53 ya kura.Bibi Royal amepata asilimia 47.Katika hotuba yake ya ushindi,Sarkozy ameahidi kuwa rais wa Wafaransa wote.Vile vile ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii. Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliompongeza Sarkozy atakaemrithi rais wa hivi sasa,Jacques Chirac hapo tarehe 16 mwezi Mei.Kansela Merkel vile vile amesema,ana hakika kuwa kiongozi mpya wa Ufaransa ataendelea kupalilia urafiki uliopo kati ya Ujerumani na Ufaransa kama kiini cha Umoja wa Ulaya.