1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy amtaka Fillion aunde serikali mpya

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqb

Rais wa Ufaransa Nicoals Sarkozy amemtaka waziri mkuu Francois Fillion aunde serikali mpya. Hatua hiyo rasmi inafuatia ushindi wa chama cha rais Sarkozy cha UMP na washirika wake kwenye uchaguzi wa bunge nchini Ufaransa.

Chama cha kihafidhina cha rais Nicolas Sarkozy kilishinda raundi ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Ufaransa kwa kupata viti 346 kati ya viti 577 bungeni.

Hata hivyo chama hicho hakikupata kura nyingi sana kama ilivyotabiriwa hapo awali. Chama cha kisoshalisiti pia kilijiimarisha kwa kupata kura nyingi katika uchaguzi huo.

Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa Iain Juppé alishindwa kupata kiti bungeni hivyo atapoteza wadhifa wake kama waziri wa mazingira na kama naibu kiongozi.

Wapigaji kura asilimia 60 walishiriki kwenye zoezi zima la uchaguzi huo.