1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy anataka kugombea urais Ufaransa

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoA

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy,ametangaza kuwa amejiandikisha rasmi kugombea uchaguzi wa urais kama mjumbe wa chama tawala cha UMP.Wagombea wengine pia wanaweza kujiandikisha hadi mwisho wa mwezi Desemba. Wanasiasa wenzake wanaotaka kugombea urais ni waziri wa ulinzi Michéle Alliot-Marie na waziri mkuu Dominique de Villepin.Chama cha Kisoshalist cha upinzani,tayari kimeshamchagua Bibi Ségolene Royal kugombea uchaguzi wa rais mwakani.