1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Ufaransa na Libya wasaini mikataba ya silaha

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcM

Kampuni kubwa kabisa ya zana za anga ya EADS imethibitisha kwamba Libya imesaini kondarasi ya kununuwa makombora ya kushambulia vifaru ya Milan yenye thamani ya karibu euro milioni 170.

Huo ni mkataba wa kwanza wa aina hiyo tokea kuondolewa kwa vikwazo vya silaha vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Libya. Mkataba wa pili wenye thamani ya euro milioni 130 umekamilishwa kwa zana za silaha na kampuni nyengine ya Ufaransa.

Saif Ul –Islam mwana wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ameliambia gazeti la Le monde kwamba kuachiliwa kwa wafanyakazi wa afya wa kigeni na serikali ya Libya wiki iliopita kumefunguwa njia ya kusainiwa kwa kondarasi kubwa za silaha na Ufaransa.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amekanusha kwamba kuachiliwa kwa wanatiba hao kumewezeshwa kutokana na makubaliano hayo ya mauzo ya silaha.