1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris: Ufaransa yamuunga mkono Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina.

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnB

Ufaransa imetangaza inamuunga mkono Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Tangazo hilo limetolewa baada ya mkutano kati ya Mahmoud Abbas na Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy mjini Paris.

Mazungumzo kati ya viongozi hao yalihusu hali jinsi ilivyo tangu chama cha Hamas kilipotwaa mamlaka ya Ukanda wa Gaza majuma mawili yaliyopita.

Mahmoud Abbas aliwasili Paris akitokea Geneva ambako mapema alitoa wito kwa watu waliohudhuria kongamano la Social International waisusie Hamas na wasaidie kuanzisha upya utaratibu wa amani ya Mashariki ya Kati.