1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS :Ulaya kuwekea Iran vikwazo vya kiuchumi

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBP6

Viongozi barani Ulaya wanapanga kuiwekea nchi ya Iran vikwazo vya kiuchumi baada ya kukataa kusitisha sehemu ya mpango wake wa nuklia.Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchner aliyeeleza kuwa vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa mataifa havijaleta mafanikio yoyote.Akizungumza na kituo cha rediocha RTL,kiongozi huyo alionya kuwa jamii ya kimataifa sharti ijiandae kwa uwezekano wa kutokea vita endapo Iran itakuwa na silaha za nuklia.Marekani na mataifa ya Ulaya wanashuku kuwa uongozi wa Iran unatafuta silaha za nuklia jambo ambalo inakanusha.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa mpango wake wa nuklia ni wa kutengeza nishati pekee.

Majadiliano aidha vikwazo vya Umoja wa mataifa vilivyowekewa Iran mara mbili havijafanikiwa kusimamisha mpango wa kurutubisha madini ya uranium ulio na uwezo wa kutengeza nishati vilevile malighafi ya kutengezea silaha za nuklia.

Wakati huohuo Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad anapendekeza kufanyika kwa mjadala wa umma pamoja na mwenzake wa Marekani George W Bush katika mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi huu.Kiongozi huyo anapendekeza kufanyika kwa kura ya maoni ya ulimwengu mzima ili kuamua aliye sahihi.

Bwana Ahmedinejad alithibitisha katika mahojiano na televisheni ya kitaifa kuwa anapanga kuhudhuria mkutano wa Baraza la Umoja wa mataifa wiki ijayo.Hii ni mara ya tatu kwa kiongozi huyo kuzuru Marekani. Rais Ahmedinejad alipendekeza mjadala kama huo alipohudhuria kikao cha mwaka jana jambo lililopuuzwa na Marekani.