1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Waasi wa kundi la ETA watiwa mbaroni

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmN

Polisi wa kupambana na ugaidi nchini Ufaransa wamewakamata washukiwa watatu wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la ETA la chama cha Basque.

Washukiwa hao walikamatwa wakati walipokuwa wakijiandaa kuvuka mpaka na kuingia Uhispania wakiwa ndani ya gari iliyokuwa imesheheni vifaa vinavyoweza kulipuka na mabomu.

Wote watatu walizuiliwa katika mji wa Saint Jean Pied de Port wakiwa na kilo 160 za vifaa vya kemikali, chupa mbili za gesi, kifaa cha kulipua mabomu na bunduki moja.

Kukamatwa kwa washukiwa hao kunafuatia kungunduliwa kwa motokaa iliyokuwa na kilo 115 za vifaa vya kulipuka iliyokuwa imeegeshwa karibu na mpaka wa Uhispania na Ureno mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Polisi wa Uhispania walikuwa wametoa onyo juu ya uwezekano wa shambulio kufanywa na kundi la ETA baada ya kundi hilo kumaliza kipindi cha miezi 14 ya usitishwaji wa mapigano.