1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Wagombea urais wako katika hatua za mwisho kuwania kura.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8k

Wagombea urais nchini Ufaransa wanafanya juhudi zao za mwisho kuwania kura kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi siku ya Jumapili. Jana Alhamis mgombea wa chama cha kihafidhina Nicolas Sarkozy aliungana pamoja na wachezaji mpira nyota pamoja na mawaziri wakuu wa zamani kwa ajili ya mkutano wake wa mwisho wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya watu mjini Marseille.

Mgombea wa chama cha Kisoshalist Segolene Royal aliungana na Danielle Mitterrand, mke wa rais wa zamani Francois Mitterrand, na waziri mkuu msoshalist wa Hispania Jose Luis Zapatero kwa ajili ya mkutano wake wa mwisho wa kampeni mjini Toulouse.

Huku maoni yakionyesha kuwa Sarkozy anauhakika zaidi wa kupata nafasi katika duru ya pili ya uchaguzi hapo May 6, duru ya kwanza siku ya Jumapili inaweza kuwa mpambano kwa ajili ya nafasi ya pili kati ya Royal na Francois Bayrou ambaye ni mfuasi wa mrengo wa kati. Zaidi ya mtu mmoja kati ya wapigakura watatu wa Ufaransa bado hawajaamua nani watampigia kura.