1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Wahafidhina washinda uchaguzi wa bunge

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsr

Wahafidhina wa Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa wameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge kwa vishindo.

Makadirio yalioandaliwa na mashirika kadhaa ya uchunguzi wa maoni yanawapa wahafidhina hao wa UMP zaidi ya asilimia 45 ya kura.Wasoshalisti na washirika wao kutoka chama cha Kijani wamejipatia asilimia 36 tu.Uchaguzi huo umeweka rekodi ya kujitokeza kwa watu wachache ambayo ilikuwa ni asilimia 60 tu.

Matokeo rasmi hayatoweza kuthibitishwa hadi hapo itakapofanyika duru ya pili ya uchaguzi huo katika kipindi kisichozidi wiki moja.

Wahafidhina wanasema kushinda kwao uchaguzi huo kutamwezesha Sarkozy kutekeleza ahadi yake ya kampeni ya uchaguzi ya kupunguza kodi katika jitihada za kukuza uchumi na kupunguza ukosefu wa ajira.