1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Waranti wa kuwakamata maafisa wakuu wa serikali ya Rwanda

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqm

Jaji kutoka nchini Ufaransa ambae anafanya uchunguzi juu ya mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyalimana katika ajali ya ndege mnamo mwaka 1994, Jean Louis Bruguière, ametoa waranti wa kukamatwa maafisa wakuu 9 wa karibu na rais wa Rwanda, Paul Kagame. Kifo hicho cha rais Habyalimana, kilikuwa chanzo cha mauaji ya kuangamiza jamii ya mwaka 1994. Shirika la habari la Associated Press, limesema jaji Jean Louis Bruguière, amepata kibali cha kutoa waranti hizo kutoka kwa wendeshamashtaka mjini Paris. Miongoni mwa wanaoshukiwa na Ufaransa ni pamoja na majenerali wawili katika jeshi la Rwanda. Familia za marubani na wafanyakazi wa ndege iliokuwa ikimsafirisha rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyalimana, walianzisha kesi mahakamani nchini Ufaransa mwaka 1998.