1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: watoto lazima walindwe katika sehemu za mizozo ya kivita

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUk

Wawakilishi kutoka nchi 60 wanakutana mjini Paris, Ufaransa kuzungumzia juu ya njia thabiti za kuwalinda watoto katika sehemu zinazokabiliwa na mizozo ya kivita.

Kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, watoto wapatao laki mbili na nusu wanatumiwa kama askari katika sehemu mbalimbali za mizozo duniani. Akizumngumza kwenye mkutano huo waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani bibi Wiezcorek Zeul ameulezea uovu wa kuwatumia watoto kama askari kuwa ni aina mbaya sana ya utumwa.