1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Waziri wa nje wa Ufaransa ziarani Irak

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXf

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner amewasili leo hii katika mji mkuu wa Irak,Baghdad.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nje ya Ufaransa mjini Paris,Kouchner anafanya ziara hiyo rasmi kuambatana na mualiko uliotolewa na Rais wa Irak,Jalal Talabani.Taarifa hiyo inasema,Kouchner amepeleka ujumbe wa ushirikiano kati ya Ufaransa na umma wa Irak.Vile vile,wakati wa ziara hiyo waziri Kouchner atasikiliza maoni ya wajumbe wa jamii zote nchini Irak.