1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Binadamu wamesababisha mabadiliko ya hewa duniani

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVu

Tume ya watafiti wa kimataifa katika mji mkuu wa Ufaransa,Paris inatazamiwa leo hii kutoa ripoti yake ya nne kuhusu hali ya hewa duniani.Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Paris,uchunguzi uliofanywa na tume hiyo ya wanasayansi huonyesha kuwa hadi mwisho ya karne,ujoto wa ardhi huenda ukaongezeka kwa sentigredi 1.8 hadi 4.5.Matokeo yake ni maafa makubwa kama kuongezeka kwa kimo cha bahari, vipindi vya ukame vitakuwa virefu zaidi na vimbunga vikali vitakavyovuma,vitasababisha hasara kubwa sana.Inasemekana kuwa binadamu kwa kama asilimia 90 ndio wamesababisha mabadiliko ya hewa duniani.