1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Jean MarieLe Pen awataka wafuasi wake wasusie uchaguzi wa duru ya Pili

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5P

Kiongozi wa mrengo wa kulia Jean-Marie Le Pen nchini Ufaransa amewataka wafuasi wake kuususia uchaguzi war ais wa duru ya pili kati ya mgombea wa kihafidhina Nicolas Sarkozy na msosholisti Segolene Royal.

Le Pen alichukua nafasi ya nne kwenye duru ya mwanzo ya uchaguzi kwa kupata kura milioni 3.8.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa jumatatu unaonyesha kuwa asilimia 89 ya wafuasi wa Le Pen watamchagua bwana Sarkozy.