1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Kampuni la Kifaransa kutialiana saini na mikubwa ya silaha na Libya

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcI

Kampuni kubwa la kutengeza silaha la eurospace limethibitisha kuwa linakaribia kutia saini mikataba miwili mikubwa na serikali ya Libya yenye thamani ya euro millioni 300.

Huu utakuwa mkataba wa kwanza wa mauzo ya silaha toka Umoja wa Ulaya ulipoiondolea Libya vikwazo vya silaha miaka mitatu iliyopita.

Habari hizo zimezua sintofahamu nchini Ufaransa, huku Rais Nicolas Sarkozy akikanusha kuwa hayo ni makubaliano ya kuachiwa kwa wauguzi wa kibulgaria waliyokuwa katika jela nchini Libya.

Wauguzi hao pamoja na daktari wa kipalestina walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha nchini Libya kwa tuhuma za kuwaambukiza mamia ya watoto virusi vya ukimwi.

Kuachiwa kwao na Libya kulifuatia juhudi za mke wa Rais huyo wa Ufaransa, Cecila Sarkozy aliyekwenda nchini Libya., ambapo baadaye rais wa Ufaransa alifanya ziara ya kiserikali nchini humo na kufunga mikataba kadhaa ya ushirikiano na taifa hilo la afrika kaskazini.