1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Marufuku kuvuta sigara hadharani nchini Ufaransa kuanzia mwakani

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4k

Ufaransa inakusudia kupiga marufuku uvutaji sigara katika sehemu zote za hadhara kuanzia mwezi februari.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo bwana Dominique de Villepin amesema sehemu zote za burudani zinapaswa kutekeleza hatua hiyo kuanzia mwezi januari . Ameeleza kuwa mtu yeyote ama sehemu yoyote ikayokiuka utararibu huo itaadhibiwa kwa kulipa faini.

Uvutaji sigara unasababisha vifo vya watu 13 kila siku nchini Ufaransa,amesema waziri mkuu huyo.