1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Mgomo wa treni na mabasi wakwamisha shughuli nchini Ufaransa

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1S

Ufaransa inakumbwa na matatizo ya usafiri huku mgomo wa wafanyikazi wa treni na mabasi ukiendelea.Mgomo huo ulianza kwa mara ya pili jana usiku ili kupinga mageuzi ya utendaji kazi na malipo ya uzeeni.Rais Nikolas Sarkozy wa Ufaransa anatangaza kurefushwa kwa muda wa kuchangia katika malipo ya uzeeni kutoka miaka 37 u nusu hadi 40 ikiwa sawa na wafanyikazi wa makampuni binafsi vilevile mengine ya umma.Kwa sasa wafanyikazi wa reli wanaruhusiwa kustaafu wakiwa na umri wa miaka 50 na kupokea malipo kamili ya uzeeni.Saa chache kabla mgomo huo wa treni kuanza Rais Sarkozy anashikilia kuwa mageuzi haoy sharti yatimizwe na kukutana na viongozi wa kampuni za reli,umeme na gesi ili kutathmini hali kwa jumla kw amujibu wa msemaji wa Rais David Martinon.

Vyama vya wafanyikazi kwa upande wao vitoa wito wa kufanyika maandamano yasiyokuwa na muda maalum wa kukamilika.Walimu na wafanyikazi wa umma wanatarjiwa kujiunga na mgomo huo wiki ijayo.

Wakazi wa mjini Paris wanalazimika kusafiri kwa baiskeli

Mgomo huo unajumuisha makampuni ya reli ya serikali,umeme na gesi. Serikali ya Ufaransa inachangia euro bilioni 5 kila mwaka katika malipo maalum ya uzeeni ili kufidia viwango vya wafanyikazi vilivyopungua.Serikali ya Ufaransa ilijaribu kuchukua hatua kama hii mwaka ’95 jambo lililosababisha migomo na maandamano yaliyodumu wiki tatu na kumlazimu Rais Jacque Chirac kubadili msimamo wake.