1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Mke wa Rais wa Ufaransa aenda Libya katika mzozo wa wauguzi

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg4

Mke wa Rais wa Ufaransa, Bi Cecilia Saxozy ameelekea Libya kushawishi kuachiwa kwa wauguzi sita waliyopatikana na hatia ya kuwaambukiza virusi vya HIV watoto zaidi ya 400 nchini humo.

Umoja wa Ulaya umethibitisha juu ya ziara hiyo ya Cecila Saxozy ambaye anafuatana na kamishna wa uhusiano wa kigeni wa Umoja huo wa Ulaya, Benita Ferrero-Waldner.

Baraza la Juu la Sheria nchini Libya wiki iliyopita lilibatilisha adhabu ya kifo waliyohukumiwa wauguzi hao watano kutoka Bulgaria na daktari mmoja wa kipalestina kuwa kifungo cha maisha.

Wanatuhumiwa kuwaambukiza virusi vya HIV watoto kiasi cha 460 katika hospitali ya Benghazi.