1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris.Muigizaji maarufu nchini Ufaransa afariki.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpq

Mchezaji nyota wa filamu nchini Ufaransa Philippe Noiret amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Wakala wa Philippe amesema, muigizaji huyo alifariki baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Noiret alikuwa ni mmoja kati ya waigizaji waliojijengea jina na kupata mafanikio katika kizazi chake, akilenga zaidi uigizaji wa filamu zilizo tamba kwa miongo mitano iliyopita, ikiwemo pia filamu aliyoigiza mwaka 1988 ijulikanayo kama “Cinema Paradiso“.