1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Rais mteule wa Ufaransa aahidi kulisaidia bara la Afrika

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC43

Rais mteule wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameahidi kuanzisha mageuzi ya kiuchumi na kisiasa nchini Ufaransa kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi wa rais wa duru ya pili uliofanyika jumapili.

Sarkozy wa chama tawala cha kihafidhina cha UMP pia ametoa wito wa kuwepo maridhiano kufuatia kampeini ya uchaguzi iliyoibua hisia kali kwa mpinzani wake wa chama cha Kisosholisti Segolene Royal.

Katika hotuba yake rais mteule bwana Sarkozy pia ameelezea malengo ya siasa yake kwa bara la Afrika.Amesema Ufaransa itakuwa tayari kuisaidia Afrika kupamabana na njaa,umaskini na vita pamoja na maradhi.

Bwana Sarkozy kwa sasa anapanga kuchukua mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kuchukua rasmi madaraka kama rais wa Ufaransa mnamo tarehe 16 Mwezi huu.Msemaji wa bwana Sarkozy ameeleza kwamba rais huyo mteule ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani atatumia muda huo kuchagua baraza lake la mawaziri.