1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Raundi ya kwanza ya uchaguzi yaanza Ufaransa

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC89

Raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais inatarajiwa kuanza baadae leo nchini Ufaransa ambapo wagombea wakuu watatu watamenyana.

Kwa mujibu wa kura za maoni, wagombea wa vyama vya kihafidhina na kisoshalisti bwana Sarkozy na bibi Royal ndio wenye mategemeo makubwa ya kushinda.

Wastahiki zaidi milioni nne watawapigia kura wajumbe 12 ili kumtafuta mrithi wa rais Chirac.