1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Segolene aihadharisha Ufaransa kutomchagua hasimu wake

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4s

Wakati leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kampeni za urais kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi, hapo siku ya Jumapili,mgombea wa chama cha kisoshalisti Bi Segolene Royal ameonya Ufaransa itakabiliwa na machafuko iwapo mpinzani wake Nicolas Sarkozy atashinda.

Bi Royal alikiambia kituo kimoja cha televisheni kuwa Sarkozy kutoka chama cha kihafidhina chenye mrengo wa kulia cha UMP ataitumbukiza Ufaransa katika mfumo wa kikatili.

Sarkozy ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani, anashutumiwa kwa kuwaita vijana waliyofanya vurugu mitaani mwaka 2005 katika miji mbalimbali ya Ufaransa kuwa ni walala hoi wasiyo na thamani.

Hata hivyo kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa bwana Sarkozy anaongoza kwa karibu asilimia nane mbele ya Bi Royal