1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Serikali za ulimwengu zatakiwa zichukue hatua juu ya hali ya anga

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVj

Ripoti ya jopo la umoja wa mataifa linalosimamia maswala ya mabadiliko ya hali ya anga imesema kuwa ongezeko la hali ya joto duniani limesababishwa na binadamu na hali hiyo itaendelea kwa karne kadhaa zijazo.

Ripoti hiyo yenye kurasa 21 iliyotayarishwa mjini Paris na jopo la watalaamu na wanasayansi 2,500, imesema kuwa kiwango cha joto ardhini kitapanda kati ya nyuzi 1.8 hadi nyuzi 4.kufikia mwaka 2100.

Kina cha bahari kitapanda kwa kiasi cha sentimita 18 na kufikia hata sentimita 59 wakati wa hali mbaya ya hewa.

Mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa aliyesimamia maswala ya mazingira Klaus Topfer amesema ripoti hiyo ni thibitisho la hali halisi linalotoa onyo kwa serikali za ulimwengu na kwamba zinahitajika kuanza kulishughulikia swala la mabadiliko ya hali ya anga.

Umoja wa ulaya umesema mazungumzo ya haraka yafanyike kufuatia ripoti hiyo ya umoja wa mataifa.

Kamishna wa maswala ya mazingira wa umoja wa ulaya Stavros Dimas amesema ametishwa na hali hiyo halisi ya kwamba asilimia 90 ya uharibifu wa mazingira inasababishwa na binadamu.