PARIS:Uchaguzi wa wabunge waendelea Ufaransa
10 Juni 2007Matangazo
Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya mwanzo kuwachagua wabunge huku chama cha rais Nicolas Sarkozy cha UMP kikitarajiwa kujiimarisha madarakani.
Sarkozy aliyechaguliwa kuwa rais wa Ufaransa mwezi mmoja uliopita kwa kunadi sera za kufanya mageuzi nchini humo anahitaji kupata ushindi wa bunge baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa bunge mnamo juni 17 ili kufanikisha mageuzi anayoyataka.
Uchaguzi wa bunge pia unafanyika nchini Ubelgiji ambako uchunguzi wa maoni unaonyesha chama cha upinzani cha Christian Demokrats kitashinda dhidi ya waliberali.