1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Ufaransa kuyaondoa mejeshi yake maalum Afghanstan

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCic

Waziri wa ulinzi nchini Ufaransa amesema Ufaransa itaondoa mamia ya wanajeshi wake wa kikosi chake maalum nchini Afghanstan.

Waziri Michele Alliot-Mariot ametoa tamko hilo mbele ya wandishi habari wakati alipofanya ziara yake mjini Kabul Afghanstan.

Kiasi ya wanajeshi 200 wakikosi maalum cha Ufaransa wako katika eneo la mashariki mwa Afghanstan ambako wanahusika kwenye operesheni ya kuhakikisha uhuru katika eneo hilo.

Ufaransa ina wanajeshi 2000 Afghanstan huku idadi nyingine ikihusika katika kikosi cha kimataifa cha usalama cha Umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO.

Tangazo la Ufaransa la kupunguza wanajeshi wake limekuja wakati makamanda wa ISAF wanatoa mwito wa kuongezwa wanajeshi katika eneo la kusini mwa Afghanstan ambako wanamgambo wakitaliban wananguvu zaidi.