1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris.Uingereza na Ufaransa zataka kupelekwa kwa haraka kwa wanajeshi Darfur.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgg

Uingereza na Ufaransa zimesema leo kuwa zitajitahidi kuweka kwa umoja wa mataifa kuidhinisha kwa haraka wanajeshi kadha na polisi kwa ajili ya jimbo la Darfur nchini Sudan.

Baada ya mkutano wao mjini Paris, rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown wamesema watatuma mawaziri wao wa mambo ya kigeni mjini New York kuunga mkono azimio la baraza la usalama .

Kwa hivi sasa , muswada wa azimio unasambazwa ili kuweza kuidhinisha wanajeshi 20,000 wa umoja wa mataifa pamoja na umoja wa Afrika kuwekwa katika jimbo la Darfur.

Brown ameitishia Sudan kuwekewa vikwazo zaidi hadi pale hatua za haraka zitakapofanyika ili kuifanya hali kuwa bora katika jimbo la Darfur, ambako kiasi cha watu 200,000 wameuwawa na wengine milioni mbili wamekimbia makaazi yao.