1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Vyombo vya usalama vyaonya kuwa huenda machaffuko yakazuka upya

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzm

Polisi na vyombo vya usalama nchini Ufaransa vimeonya kuwa huenda machafuko yakazuka upya katika maeneo duni yanayoishi raia wengi wa kigeni katika vitongoji vya mji wa Paris.

Gazeti la kila siku la Le Figaro limechapisha waraka wa siri mwaka mmoja baada ya Ufaransa kukumbwa na wiki tatu za machafuko na ghasia katika vitongoji kadhaa vya mji wa Paris.

Waraka huo umeeleza kuwa sababu zilizochochea ghasia za mwaka uliopita bado hazijasuluhishwa.

Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa sababu kubwa zilizochochea machafuko ni umasikini, ukosefu wa ajira na ubaguzi.

Siku mbili zilizopita vijana walilichoma moto basi nje ya mji wa Paris na waliwapiga kwa mawe polisi na wazima maoto waliofika katika sehemu ya tukio.