1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PAU, UFARANSA: Aliyekuwa akiongoza mashindano ya baiskeli atimuliwa

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBf7

Aliyekuwa akiongoza mashindano ya kuendesha baiskeli, Tour de France, Michael Rasmussen, amefutwa kazi na timu yake na kuondolewa kwenye mashindano.

Msemaji wa timu ya mashindano ya baiskeli ya Danemark ya Rabobank, amesema Rasmussen ametimuliwa kwa kuvunja sheria za timu hiyo.

Rasmussen alimdanganya mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo kuhusu alikokuwa mwezi uliopita, baada ya kukosa kupimwa damu kubaini ikiwa anatumia dawa za kuongeza nguvu misuli.

Imeripotiwa mwendesha baiskeli huyo alisema alikuwa nchini Mexico ilhali alikuwa nchini Italy.

Rasmussen mwenye umri wa miaka 33 alikosa mara mbili kupimwa kabla ya mashindano na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mashindano ya Tour de France baada ya kushinda awamu ya 16 kwenye mashidano ya Col d´Aubisque.

Kuondolewa kwa Rasmussen ni pigo kubwa miongoni mwa kashfa zilizoyakabili mashindano ya kuendesha baiskeli mwaka huu na mchezo huo kwa jumla.