1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paul Pogba ana mambo mengi ya kuonesha

Sekione Kitojo
12 Novemba 2016

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps anasisitiza kwamba kuna mambo mengi zaidi katika mchezo wa Paul Pogba kuliko kufunga mabao kwa timu ya taifa ya Ufaransa. Pogba alifunga bao dhidi ya Sweden.

https://p.dw.com/p/2SanT
Fußball WM 2014 Deutschland Frankreich Viertelfinale
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier DeschampsPicha: Reuters

Kocha  wa  Ufaransa  Didier  Deschamps anasisitiza  kwamba  kuna mambo  mengi  zaidi  katika  mchezo  wa  Paul Pogba  baada  ya mchezaji  huyo  wa  Manchester  United  kufunga  bao  tena  katika ushindi  wa  mabao  2-1  dhidi  ya  Sweden  jana Ijumaa(11.11.2016).

Mchezaji  huyo  ghali  kabisa  duniani  alifunga  kwa  kichwa  katika ushindi  huo  wa  Ufaransa , ambapo  Dimitri Payet  aliunga  bao  la ushindi  katika  mchezo  wa  kufuzu  kucheza  katika  fainali  za kombe  la  dunia  katika  uwanja  wa  Stade de France nchini Ufaransa.

Ni  bao  la  nane  la  Pogba  kwa  nchi  yake  na  linafuatiwa  na  bao la  ushindi  alilofunga  ugenini  dhidi  ya  Uholanzi mwezi uliopita.

UEFA Euro 2016 Frankreich gegen Island Tor Jubel Pogba
Mchezaji wa kati wa Ufaransa Paul PogbaPicha: Reuters/C. Hartmann

Pogba  mwenye  umri  wa  miaka  23 pia  alifunga  bao  safi  katika ushindi  wa  mabao  3-1  wa  timu  yake  ya  United  dhidi  ya Swansea  katika  ligi  ya  Uingereza  Premier  League mwishoni mwa  juma  lililopita  lakini  Deschamps  alisema: "Si mfungaji mabao. Anaweza  kufunga  mabao  na  ameweza  kufanya  hivyo lakini  simtarajii  kufanya  hivyo.

"Ni  vizuri  alivyofanya  leo  lakini  ninafurahi  zaidi  kwa  jinsi alivyocheza hali  ambayo  inafuatia  mchezo  mzuri  aliocheza Uhloanzi.

"Kwa Manchester  anatumika  katika  nafasi  nyingine  katika  mfumo tofauti. Alitupa  uwezo  mkubwa  wa  kucheza  mpira  na  alikuwa mzuri  katika  kunyang'anya  mipira," Deschamps aliongeza.

"Wakati  Paul  akicheza  kama  hivi  na  anashirikiana  vizuri  na Blaise Matuidi  ni  muhimu  kwa  timu. Iwapo  anafunga  mabao , ni vizuri  zaidi. Nafahamu  anapenda  kufunga  lakini  si  kitu  ambacho mimi  pamoja  na  timu  tunakitarajia  kutoka  kwake."

Ufaransa  inaongoza  kwa  pointi  tatu  dhidi  ya  Sweden  katika kundi  A ikiwa  imebakia  michezo  minne  katika  duru  ya  Ulaya  ya kufuzu  kucheza  katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka  2018 nchini  Ufaransa.

 

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Sylvia  Mwehozi