1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PEKING: Mkutano utaathiri uhusiano wa Marekani na China

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FL

China imeonya,mkutano uliopangwa kufanywa baadae leo hii kati ya Rais George W.Bush wa Marekani na Dalai Lama katika Ikulu ya Marekani,utaathiri vibaya sana uhusiano wa Marekani na China. Kiongozi wa kidini wa Tibet anaeishi uhamishoni yupo ziarani mjini Washington na siku ya Jumatano atatunikiwa Medali ya Dhahabu ya Bunge.

Hivi karibuni pia;uhusiano wa China na Ujerumani ulikuwa na mvutano,baada ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kumpokea Dalai Lama mjini Berlin. China,tangu miaka mingi inamuona Dalai Lama kama ni kitisho kwa usalama wa ndani,kwa sababu kiongozi huyo wa kidini,anaendelea kugombea utawala wa ndani wa Tibet.