1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PEKING:kimbunga "Dean" kipo njiani kuelekea Jamaika

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXs

Watu zaidi ya milioni moja wamekimbilia kwenye sehemu za usalama kwenye pwani ya kusini mashariki mwa China ili kuepuka kimbunga Sepat.

Katika jimbo la Fuji pekee watu zaidi ya laki tano wamehamishwa. Watabiri wa hali ya hewa wametahadharisha juu ya hatari kubwa ya kimbunga hicho ambacho tayari kimeshazikumbuka sehemu za Taiwan.

Na katika nchi za eneo la karibik kimbunga Dean kimeshauwa watu kadhaa.

Nchini Jamaika watu wamelazimika kulimbikiza akiba za mahitaji kutokana na tishio la kimbunga Dean ambacho kimefikia kasi ya kilometa 240 kwa saa.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuikumba nchi hiyo leo.