1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR : Mripuko wauwa 15

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXG

Takriban watu 15 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika kile kinachoonekana kuwa shambulio la kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa karibu na msikiti wa Washia katika mji wa kaskazini mwa Pakistan wa Peshawar.

Taarifa zinasema mkuu wa polisi wa eneo hilo na askari 12 ni miongoni mwa waliouwawa baada ya mripuko wenye nguvu kubwa kutingisha barabara iliokuwa imepangwa kupita maandamano ya kidini.

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amelaani shambulio hilo na ameamuru kufanyika uchunguzi.

Peshawar iko Jimbo la Mpaka wa Kaskazini Magharibi ambalo hupakana na Afghanistan na umekuwa na ongezeko la machafuko katika miaka ya hivi karibuni.