1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Phnom Penh. Kiongozi wa Khmer Rouge akamatwa.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOS

Nchini Cambodia kiongozi wa ngazi ya juu aliyebaki wa kundi la Khmer Rouge , Noun Chea amekamatwa katika msitu karibu na mpaka wa Thailand na kupelekwa mjini Phnom Penh , ambako atafikishwa mbele ya mahakama inayoungwa mkono na umoja wa mataifa. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 anadaiwa kuwa ndie aliyekuwa anapanga sera za mauaji na mshauri wa karibu wa Pol Pot, kiongozi wa kundi hilo ambaye alifariki mwaka 1998. Nuon Chea amekana kuhusika na mauaji. Utawala huo wa zamani uliwakamata watu kutoka mijini katika miaka ya 1970 wakati wakijaribu kujenga nadharia za uchumi wa kilimo. Kiasi cha zaidi ya Wakambodia milioni mbili walifariki kutokana na njaa, kazi za kupita kiasi na mauaji. Mahakama hiyo iliyoundwa mwaka jana hadi sasa imemshitaki mtuhumiwa mmoja, Khang Khek, ambaye anadaiwa alikuwa mkuu wa kituo cha kuwatesa watu.