1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Podolski kukosa mpambano dhidi ya Algeria

29 Juni 2014

Lukas Podolski atakosa mchuano ujao wa kufuzu katika robo fainali dhidi ya Algeria utakaochezwa Jumatatu (30.06.2014). Kocha Joachim Löw pia amesema beki Jerome Boateng bado hayuko 'fit'

https://p.dw.com/p/1CSB4
WM 2014 Deutschland Lukas Podolski Training
Picha: picture-alliance/dpa

Löw amewaambia waandishi habari katika kambi ya mafunzo ya Ujerumani ya Santo Andre kuwa Podolski hatakuwa tayari kwa wakati unaofaa kucheza mpambano wa Algeria, akisema kuwa mchezaji huyo wa pembeni wa Arsenal atastahili kupumzika kwa siku mbili au tatu.

Kocha huyo wa Ujerumani amesema “inaweza kuwa hatari kubwa” kumjumuisha Podolski kikosini katika mpambano huo wa Jumatatu, kwa sababu unaweza kuathiri jeraha lake hata zaidi. Anaweza kuwa tayari kwa mechi nyingine kama watafuzu.

Beki Jerome Boateng amepata jeraha jingine, mara hii akiumia katika goti lake la kushoto. Löw amesema jeraha hilo siyo ba ya sana.

Dhidi ya Algeria, Ujerumani inapambana na timu dhabiti zaidi ya Afrika katika dimba hilo kufikia sasa. Löw amesema Desert Warriors ni “hatari mno na wenye nguvu uwanjani” na hivyo haitakuwa kazi rahisi kwa vijana wake, lakini akaongeza kuwa timu yake inaweza kuimarika baada ya kutoka sare na Ghana na kuwapiku kwa ushindi mdogo sana timu ya Marekani yake Jürgen Klinsmann katika hatua ya makundi.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/DW/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo