1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yaota kufanya makubwa Uefa, Euro 2012

8 Juni 2012

Ijumaa (08.06.2012) ni siku ya ufunguzi rasmi wa mashindano haya yanayosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki kote duniani, ya Uefa,Euro 2012, Poland na Ukraine zikiwa wenyeji wenza.

https://p.dw.com/p/15AC1
Poland's team is seen prior to a test soccer match between Poland and Belarus in Wiesbaden, Germany, Tuesday, Oct.11, 2011. The draw for the final tournament of the Euro 2012 is to be held on Friday, Dec. 2, 2011 in Kiev, Ukraine. (Foto:Michael Probst/AP/dapd)
Kikosi cha timu ya taifa ya PolandPicha: dapd

Poland wenyeji  wenza  wa  mashindano  haya  wana ndoto za kupata  mafanikio  makubwa  na  sio tu  kwasababu  wao  ni wenyeji, pamoja  na  kwamba   jukumu  hilo  linatoa  hamasa  kubwa. Lakini enzi  za  mafanikio  makubwa  ya  soka  kwa  Poland  zimepita, ambapo  mafanikio  pekee  makubwa  ni  katika  mwaka  1974  na 1982 , ambapo nchi  hiyo  ilishika  nafasi  ya  tatu  katika  fainali  za kombe la dunia.

Poland  katika  miaka  ya  hivi  karibuni ilidorora na  kuyaaga mashindano  ya  fainali  za  kombe  la  dunia na  kombe  la  mataifa ya  Ulaya  katika  duru  za  mwanzo.

Kocha Franciszek Smuda  ana  kibarua  kigumu  mbele  yake. Kundi hili  la  A linatimu  zinazolingana  kiuwezo, lakini  hii  haina  maana  ya kuondoa  hamasa  kwa  Poland. Kocha  Smuda  anawategemea sana  wachezaji  wake  nyota  wa  mabingwa  mara  mbili  nchini Ujerumani  na  mabingwa  wa  kombe  la  shirikisho, DFB Pokal , Borussia  Dortmund. Jakub , Kuba , Blaszcykowski,  Lukasz Piszczek na  mshambuliaji Robert  Lewandowski  ni  nyota  wanaong'ara nchini  Poland.

Fußball,Fussball, International, 11.11.2011 Freundschaftsspiel: Polen - Italien 0:2 Einzelaktion ROBERT LEWANDOWSKI
Mshambuliaji wa Poland Robert LewandowskiPicha: picture alliance/augenklick/firo Sportphoto

Hii  itakuwa historia  kubwa  kwa  nchi  yetu, amesema  mlinzi  wa Borussia  Dortmund  na  Poland, Lukasz Piszczek,  akiwa  na  furaha kubwa. Nahodha  Kuba Blaszcykowski  anatoa  lengo  la timu  yake kuwa  ni  kufika  robo fainali  kwanza. Kabla  ya  hapo,  lakini,  kuna kibarua  dhidi  ya Ugiriki  hapo  Ijumaa Juni 8 mjini  Warsaw wakati wa  ufunguzi  wa  mashindano  hayo.

Huu  ndio  mchezo muhimu  sana  kwetu. Kabla  ya  mashindano haya  ya Euro  2012, kulikuwa  na  hali  ya  wasi  wasi  kutokana  na kashfa  ya rushwa pamoja  na utata  dhidi  ya  mlinzi  Piszczek katika kashfa  ya  kupanga  matokeo  katika  kikosi  hicho  cha  Poland. Smuda  pamoja  na  hayo  amemuita mlinzi  huyo  katika  kikosi hicho na  kumtupa  nje  ya  kikosi  Slawomir Peszko  kutoka  FC Köln  kutokana  na  kashfa  ya  ulevi.

Katika  orodha  ya  timu  bora  duniani, Urusi  imo  katika  nafasi  ya 11 na ni timu  inayoonekana  kuwa  na  nafasi  kubwa  ya  kuvuka kiunzi  hicho  cha  makundi, na  kufuatiwa  na  Ugiriki  iliyo  katika nafasi  ya  14  katika  orodha  ya  timu  bora  duniani. Lakini  Urusi kukosa  kufuzu  kucheza  katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka 2010  kuliwahuzunisha  sana. Wakati  huo  kikosi  cha  kocha  Guus Hiddink  kilikwama  katika  michezo  ya  awali  ya  kufuzu  kucheza fainali  hizo  na  kocha huyo alifungishwa  virago   na  kurejea  kwao Uholanzi. Matarajio  kwa  mrithi  wa  kiti  cha  Hiddink, Dick Advocaat,  ni  makubwa. Lakini  hata  hivyo Advocaat yuko  njiani kukiacha  mkono  kikosi  hicho  cha  Urusi  kwani  anarejea nyumbani  baada  ya  mashindano  haya,  tayari  kushika  usukani wa  kukiongoza  kikosi  cha  timu  ya daraja  la  kwanza  nchini Uholanzi ya  PSV Eindhoven.

Soccer_Euro_2008_Pr_7244986.jpg ** Soccer Euro 2008 Preview ** Greece's national soccer team is pictured prior to the friendly soccer match between Portugal and Greece in Duesseldorf, Germany, Wednesday, March 26, 2008. Up from left: Paraskevas Antzas, Konstantinos Katsouranis, Angelos Charisteas, Sotirios Kyrgiakos, Antonios Nikopolidis , Angelos Basinas. Down from left: Theofanis Gekas, Christos Patsazoglou, Georgios Karagounis, Ioannis Amanatidis, Vassilis Torosidis. (AP Photo/Martin Meissner)
Timu ya taifa ya UgirikiPicha: AP

Advocaat  amekiongoza  kikosi  cha  Urusi kupitia  nahodha  Andrej Arschavin  na  mshambuliaji Pavel Pogrebnjak, katika  awamu  ya kufuzu  kucheza  fainali  hizi  na  ana  matumaini , kwamba ukosoaji dhidi  ya  timu  hiyo  ya  taifa  utakuwa  umepitwa  na  wakati.

Ugiriki,  chini  ya  kocha  wao Mjerumani,  Otto Rehhagel , ilitawazwa mabingwa  wa  Ulaya  mwaka  2004, lakini  tangu  wakati  huo  kikosi hicho  hakijaonyesha  makali  yake ya  hapo  zamani. Fernando Manuel Costa Santos  anatafuta  mbinu  za Rehhagel  za ukuta pamoja  na  wachezaji  wakongwe , kama Theofanis Gekas, kuleta mafanikio  katika  timu  hiyo. Kocha  huyo  wa  taifa  la  Ugiriki anaweza  kupata  mafanikio , kupitia  nyayo  alizopitia  mtangulizi wake Otto  Rehhagel.

Jamhuri  ya  Czech  iliwahi  kuvuma. Majina  yaliyobaki  katika kumbukumbu  ni  kama  Pavel  Nedved na  Karel  Poborsky, lakini pia  bado wapo  mlinda  mlango  wa  Chelsea  London, Petr Cech, na  Tomas Rosicky  wa  Arsenal London. Mwaka 1976 iliyokuwa Yugoslavia ya zamani  ilitawazwa  mabingwa  wa  kombe  la  Ulaya na  mwaka  2004 Jamhuri  ya  Czech  iliyokuwa  sehemu  ya Yugoslavia , ilifikia  nusu  fainali  ya  kombe  la  Euro. Tangu  wakati huo  jamhuri  ya  Czech  imekuwa katika  nafasi  za kati kwa  kati. Lakini  sasa  kocha Michal Bilik  ameibadilisha  sana  timu  hiyo, kwa kuwapa  nafasi  vijana  wengi  chipukizi na  ana  matumaini  kuwa kikosi  hicho  kitanusurika  katika  duru  hii ya  makundi.

Mwandishi : Olivia Fritz / ZR/ Sekione  Kitojo

Mhariri : Othman  Miraji.