Polisario kuendeleza mapambano ya silaha
15 Desemba 2007Matangazo
ALGIERS
Kiongozi wa chama kinachogombania uhuru wa Sahara Magharibi amesisitiza haja ya mapambano ya silaha dhidi ya Morocco.
Katibu Mkuu wa chama cha Polisario Mohamed Abdelaziz ameauambia mkutano mkuu wa siku tano wa chama hicho ulioanza hapo jana katika eneo linalogombaniwa kwamba wanaendesha vita vya ukombozi ambavyo vitaendelea hadi hapo yatakapofanikiwa malengo yaheshima.
Ameongeza kusema kwamba azimio la kimataifa linahalalisha mapambano yao ya kutetea haki zao kwa kutumia njia zozote zinazowezekana kwa upinzani wa amani na kwa mapambano ya silaha.