1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi afungwa miaka 10 Misri

Sekione Kitojo
19 Juni 2017

Mahakama nchini Misri leo imemhukumu polisi kwenda jela miaka 10 kwa  kumuua  mwanaharakati wakati  wa maandamano kumbukumbu  ya  mwaka  wa  nne  wa vuguvugu  la  umma  mwaka  2011.

https://p.dw.com/p/2exhq
Ägypten Polizei Tal der Könige
Picha: picture-alliance/dpa/O. Weiken

Mahakama  nchini  Misri leo imemhukumu  polisi kwenda jela  miaka  10 kwa  kumuua  mwanaharakati wakati  wa maandamano  ya  kumbukumbu  ya  mwaka  wa  nne  wa vuguvugu  la  umma  mwaka  2011.

Luteni Yaseen Hetem  alishitakiwa  Machi 2015 kwa kuhusika  na  hatua  ambayo  ilisababisha  kifo cha Shaimaa Sabbagh  mwenye  umri  wa  miaka  32, kosa dogo  kuliko  kuuwa, lakini  bado  ni  hatua  isiyo  ya kawaida  kwa  mzinzi  wa  usalama.

Jaji Ahmed Aboul Fotouh Sulieman wa  mahakama  ya kusini  mwa  Cairo alisoma  hukumu  hiyo  leo. Mahakama nyingine  hapo  kabla  ilimhukumu  Hatem  kwenda  jela miaka  15  mwezi  Juni  2015, lakini  hukumu  hiyo ilibadilishwa  na  mahakama  maalum  ambayo  iliamuru kesi  hiyo  irudiwe mwezi Februari  mwaka  2016.

Hatem  anaweza  kukata  rufaa  dhidi  ya  hukumu  hiyo katika  mahakama  maalum  ya  Misri , ambayo  inaweza kukubali  hukumu  ama  kuamuru  kesi  kurudiwa kwa mara  nyingine  na  ya  mwisho.