1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani wapinga kuondosha udhidbiti mpakani

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS9V

Mamia ya maafisa wa polisi Ujerumani ya mashariki wamepinga mipango ya kuondowa udhibiti wa mipakani mwezi ujao.

Chama cha wafanyakazi cha polisi kinamtaka Waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble kuendelea kuwabakisha polisi wa serikali ya shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwenye mpaka hadi hapo utakapokuwa umefanyika uchambuzi wa usalama unaoaminika.

Schäuble amezikataa shutuma hizo kwa kusema kwamba kufunguliwa mpaka kwa nchi jirani za mashariki hakutopunguza kiwango cha usalama nchini Ujerumani.

Schäuble anasema hiyo ni dhamira njema kwamba tarehe hiyo 21 Desemba italeta uhuru wa kiwango kikubwa lakini sio uchache wa usalama kwa watu wa pande mbili za mpaka na utakuwepo usalama zaidi na maalum.

Upingaji huo usio ya kawaida wa polisi unaonyesha hofu nchini Ujerumani juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa uhalifu au kumiminika kwa wimbi kubwa la wahamiaji wasio halali wakati mpaka huo utakapofunguliwa hapo tarehe 21 Desemba.