Polisi Ujerumani yawatia mbaroni washukiwa wa ugaidi
1 Februari 2017Matangazo
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa washukiwa hao walikuwa wanapanga shambulizi kubwa la kigaidi. Aidha polisi walivamia msikiti mmoja ulioko katika eneo la Moabit mjini Berlin ambako watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwa mazungumzo. Watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Desemba 19 mwaka jana katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na raia mmoja wa Tunisia Anis Amri baada ya kuendesha lori katika soko la Krismasi mjini Berlin lililokuwa limefurika watu hali iliyopelekea serikali ya Ujerumani kuchukua hatua za kuimarisha usalama.
Mwandishi: Isaac Gamba/dw
Mhariri: Gakuba Daniel