1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi waendelea na msako wa wezi wa mifugo nchini Kenya

14 Novemba 2012

Polisi nchini Kenya bado inaendelea na harakati za kuwasaka wezi wa mifugo waliosababisha mauaji ya takriban polisi 42 katika eneo la Baragoi kaskazini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/16iwQ
Mifugo nchini Kenya
Mifugo nchini KenyaPicha: AP

Polisi wengine zaidi ya 20 wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini humo. Maafisa hao wa polisi walikuwa katika harakati za kuwatafuta n'gombe walioibiwa wakati waliposhambuliwa na wezi wa mifugo.

Tayari polisi ya Kenya imetangaza vita dhidi ya wezi wa mifugo na maafisa kadhaa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo kuendeleza msako mkali wa majangili hao.

Kutaka kujua zaidi juu ya hali ilivyo huko Amina Abubakar amezungumza na kamishna wa polisi katika eneo hilo Osman Warfa.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Yusuf Saumu