1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wanane wauawa Iraq

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYYi

BAGHDAD.Mtu mmoja anayehisiwa kuwa mwanamgambo wa al Qaeda amewaua polisi wanane wa Iraq kwa kuwapiga risasi walipokuwa katika kituo cha ukaguzi kwenye jimbo la Diyala.

Katika mji wa Tappah kiasi cha kilometa 130 kaskazini mwa Baghdad maafisa saba wa polisi walijeruhiwa kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa kisunni.

Wapiganaji hao wa kisunni na al Qaeda wamejiimarisha katika maeneo ya kaskazini mwa Baghdad baada ya kufurushwa kutoka magharibi katika jimbo la Anbar kutokana na harakati kubwa zinazoendeshwa na majeshi ya Marekani.