1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wapambana na waandamanaji.

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSbz

Kampala. Polisi wa Uganda wamepambana na waandamanaji kandoni mwa mkutano wa jumuiya ya madola, Commonwealth , katika mji mkuu wa Uganda , Kampala. Afisa mmoja wa polisi na muandamanaji mmoja walijeruhiwa vibaya baada ya polisi kuwapiga virungu waandamanaji wanaopinga dhidi ya kuendewa kinyume haki za binadamu nchini humo. Baadhi ya waandamanaji walijibu kwa kurusha mawe na chupa kwa polisi. Maafisa wa usalama wametetea hatua hiyo kwa kusema kuwa kundi hilo la waandamanaji limeondoka kutoka katika eneo rasmi la maandamano. Wapinzani wa rais Yoweri Museveni wanaishutumu jumuiya ya madola kwa kupuuzia haki za binadamu nchini Uganda.