1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Ujerumani yawasaka wanachama wa Reichbürger

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Misako imefanyika katika majimbo ya Bavaria, Baden-Württemberg, Hesse, North Rhine Westphalia, Rhineland-Palatinate na Thuringia.

https://p.dw.com/p/4XMAj
Wafuasi wa vuguvugu la Reichbürger hawatambui uhalali wa serikali ya Ujerumani na wanapinga taasisi zake za demokrasia kama vile bunge na mahakama.
Wafuasi wa vuguvugu la Reichbürger hawatambui uhalali wa serikali ya Ujerumani na wanapinga taasisi zake za demokrasia kama vile bunge na mahakama.Picha: Fricke/NEWS5/AFP

Polisi ya Ujerumani imefanya msako katika majimbo kadhaa kwenye nyumba za wanachama wa vuguvugu la misimamo mikali ya mrengo wa kulia la Reichbürger na kuwakamata washukiwa kadhaa.

Hayo ni kwa mujibu wa Afisi ya mwendesha mashitaka wa umma mjini Munich.

Afisi hiyo imesema mshukiwa mmoja alikuwa amepanga kwenda kushiriki njama ya kumteka nyara waziri wa afya Karl Lauterbach na kupata silaha kwa ajili ya kazi hii nchini Croatia.

Wafuasi wa vuguvugu la Reichbürger hawatambui uhalali wa serikali ya Ujerumani na wanapinga taasisi zake za demokrasia kama vile bunge na mahakama.

Wanamdharau waziri Lauterbach kwa vizuizi ambavyo serikali iliviweka wakati wa kilele cha janga la corona.

Misako imefanyika katika majimbo ya Bavaria, Baden-Württemberg, Hesse, North Rhine Westphalia, Rhineland-Palatinate na Thuringia.

Polisi pia wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kwa kulipa kundi hilo sava kwa ajili ya mawasiliano na kushiriki kusimamia kundi la siri la mawasiliano kupitia taarifa fupi za maandishi.