1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi yavamia ofisi za MDC Harare

Kalyango Siraj25 Aprili 2008

MDC yadai polisi inaficha ushahidi

https://p.dw.com/p/DogY
Wafuasi wa chama cha upinzani Zimbabwe cha Movement for Democratic Change, MDC, wakipelekwa na polisi nje ya ofisi za chama hicho katika jengo lao Harare, Ijumaa April 25, 2008.Picha: AP

Polisi ya kuzuia fujo nchini Zimbabwe imeyavamia makao makuu ya chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change MDC yalioko katika mji mkuu wa Harare na kuwachukua watu kadhaa.

Polisi inasema waliokamatwa ni washukiwa wa makosa mbalimbali waliotenda hivi majuzi katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.Upande wa upinzani unasema wengi wa waliokamatwa walikuwa wanahifadhiwa hapo baada ya kuandamwa na wafuasi wa chama tawala.

Watu waliokamatwa katika operesheni hiyo ya polisi ni takriban 300.Na inasemekana kuwa hii ndio mara ya kwanza ya chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change,MDC,kuandamwa hivyo tangu uchaguzi unaotatanisha ufanyike mwezi jana nchini humo.

Mwandishi wa habari wa shirika la Reuters,alieshuhudia operesheni hiyo anasema kuwa polisi kadhaa wa kuzuia fujo wamewakamata wafuasi wa chama cha MDC karibu 100 baada ya kuwaingiza kwenye mabasi yaliyokuwa yamejaa watu wengine.

Msemaji wa Polisi,Wayne Bvudzijena amenukuliwa kusema kuwa waliokamatwa ni washukiwa wa makosa tofauti yaliyofanyika katika sehemu mbalimbali nchini humo.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la kijerumani DPA alieshuhudia anasema kuwa aliona askari 50 wa polisi wakifanya.

Lakini chama cha MDC kinatoa idadi tofauti ya askari polisi.Kinasema waliohusika walikuwa 250.Kinaongeza kuwa mbali na kuwakamata wafuasi pamoja na watumishi wao kadhaa na pia polisi ilizipeleka kompyuta ambazo zilikuwa zinatumiwa na na kitengo chao kilichokuwa kinafuatilia uchaguzi mkuu.

Msemaji wake anasema jengo hilo lilikuwa na watu 300 wakati kamatakamata hiyo ilipotokea leo Ijumaa.

Msemaji wa MDC,Nelson Chamisa amesema kuwa utawala wa sasa unajaribu kuficha ushahidi wa vitendo vya ghasia na fujo.

Polisi ikisema kuwa kuwa operesheni hiyo ililengwa wale tu waliojificha katika makao makuu ya chama hicho baada ya kufanya makosa nje ya mji wa Harare. Polisi imeendelea kuwa wote sio watumishi wa ofisi hiyo.Aidha msemaji huyo wa Polisi amesema kuwa kuna kesi zinazochunguzwa na baadhi ya wale waliokamatwa ikiwa watakuwa hawahusiki wataachiliwa huru.

Chama cha MDC kinadai kuwa kiongozi wake Morgan Tsvangirai alimbwaga rais mugabe katika uchaguzi wa Machi 29 ambapo matokeo yake hadi sasa hayajatangazwa na tume ya uchaguzi inayosimamiwa na serikali.

Kucheleweshwa huko kutoa matokeo ya ucchaguzi wa urais kumeleta wasiwasi miongini mwa watu mbalimbali na pia gazeti la serikali katika toleoa moja katika safu ya maoni kupendekeza kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ikijumulisha vyama vya ZANU PF kilichoko madarakani na MDC.Pendekezo hilo linaendelea kuwa,serikali hiyo iwe inaongoza na rais Mugabe.Mfumo huo inaonekana unapingwa na kingozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Utawala wa Mugabe unamlaumu Tsvangirai kwa kuwa kibaraka wa mataifa ya magharibi sanasana Uingereza na Marekani.Mwanadiplomaisa wa Marekani anaehusika na Afrika Jendayi Frazer alisema jana kuwa upinzani ulishinda uchaguzi na kuongeza kuwa nchi yake inaunga mkono mwito wa mkoloni wa zamani wa Zimbabwe, Uingereza wa kuuwekea utawala wa Mugabe vikwazo vya silaha.

Lakini gazeti la serikali ya Zimbabwe la The Herald limeandika kuwa taifa linahitaji silaha kwa ajili ya kujilinda dhidi ya uvamizi.