1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM: Mkutano wa maandalizi ya mkutano wa kilele wa nchi za G8 wafanyika

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwf

Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani, pamoja na waziri wa kigeni kutoka Urusi, wanakutana mjini Potsdam hapa Ujerumani kuandaa mkutano wa kilele wa nchi za G8.

Mkutano huo, utatuwama juu ya mzozo wa nyuklia wa Iran, mabadiliko ya hali ya hewa, hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo na machafuko nchini Irak, Afghanistan, Darfur na Mashariki ya Kati.

Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka Pakistan na Afghanistan watahudhuria mazungumzo hayo kama sehemu ya juhudi za Ujerumani. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani amesema lengo la mazungumzo hayo ni kuboresha ushirikiano baina ya Pakistan na Afghanistan katika kupambana na wanamgambo wa kiislamu.

Baadaye leo pande nne zinazoudhamini mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, zikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi, zitakutana mjini Berlin kujadili mchakato wa amani baina ya Israel na Wapalestina.