1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM UJERUMANI: Wajerumani watangaza urafiki na wazanzibar

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLC

Halmashauri ya mji wa Potsdam, imetangaza kuanzisha ushirikiano wa kidugu na mji wa Zanzibar nchini Tanzania.

Uamuzi huo ulifikiwa jana usiku katika kikao cha wakuu wa Halmashauri ya mji huo, uliyo jirani na jiji la Berlin.

Mji wa Potsdam ni makao makuu wa jimbo la Brandburg nchini Ujerumani na tena unawavutia watalii wengi kutokana na historia yake.