1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Potsdam, Ujrumani. Mkutano wa mataifa yanayoendelea na yale tajiri wavunjika.

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpY

Mazungumzo ya biashara yanayofanyika nje kidogo ya mji wa Berlin nchini Ujerumani yamevunjika.

Marekani, umoja wa Ulaya , Brazil na India zilikuwa zinakutana kujaribu kuondoa tofauti zao baina ya nchi tajiri na zile zinazoendelea kabla ya mkutano wa shirika la biashara ya dunia WTO baadaye mwaka huu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Brazil Celso Amorin amesema kuwa ujumbe wa mataifa ya India na Brazil umetoka nje ya mkutano huo kwa sababu mazungumzo yameonekana kutokuwa na faida yoyote

Amesema kuwa walichokuwa wanahitaji kutoka mataifa tajiri kilikuwa ni zaidi ya kile wanachoweza kukitoa. Na kile mataifa hayo tajiri yanachodai kutoka mataifa yanayoendelea hakikuweza kufikiwa katika hatua wanayoihitaji, na kwamba mataifa hayo yamezoea kupata kile wakitakacho kutoka mataifa yanayoendelea.

Mataifa yanayoendelea yanataka punguzo la ruzuku za kilimo kwa mataifa ya Marekani na umoja wa Ulaya ili kuweza kupata nafasi zaidi ya kuingia katika sekta za viwanda na huduma za nchi zinazoendelea.